Bado moja tutinge Robo Fainali Afrika

Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata leo dhidi ya El Merrikh umetufanya kubakisha alama moja ili kuingia hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Katika mchezo wa leo uliofanyika katika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Luis Miquissone alitupatia bao la kwanza dakika ya 18 akimalizia mpira uliopigwa na Clatous Chama baada ya walinzi wa El Merrikh kuzembea kuondoa hatari.

Mohammed Hussein aliongeza bao la pili dakika ya 39 kwa shuti kali la chini chini kutoka upande wa kushoto baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Bernard Morrison.

Mlinzi Joash Onyango alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 45 baada ya kupata maumivu.

Chris Mugalu alitupia bao la tatu dakika ya 49 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Miquissone.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Onyango, Mzamiru Yassin, Mugalu na Miquissone na kuwaingizia Erasto Nyoni, Rally Bwalya, Medie Kagere, Jonas Mkude na Francis Kahata.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 10 tukiendelea kuongoza kundi A huku tukibakiwa na mechi mbili ambazo tutakiwa kupata alama moja na kutinga moja kwa moja robo fainali bila kuangalia wengine wamefanya nini.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER