Babacar Sarr ni Mnyama

Tumemsajili kiungo mkabaji, Babacar Sarr raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 26 kutoka US Monastir kwa mkataba wa miaka miwili.

Sarr ni kiungo mwenye uzoefu wa kucheza soka la Afrika ambapo mbali na Monastir amewahi kuzichezea Olympique Beja ya Tunisia, Teungueth FC, AS Pikine na Mbour P.C.

Sarr ana uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mkabaji na wakati mwingine anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji kwahiyo ni jambo ambalo limetuvutia.

Sarr anakuja kuungana na viungo wakati kama Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis.

Sarr anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika dirisha hili la usajili baada ya kiungo Salem Karabaka ambaye tumemsajili kutoka JKU ya Zanzibar mwanzoni mwa wiki hii.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER