Babacar aanza mazoezi Zanzibar

Kiungo mpya mkabaji, Babacar Sarr ameanza mazoezi ya utimamu wa mwili ili kujiweka sawa kabla ya kujiunga moja kwa moja na wenzake.

Babacar amekamilisha usajili wake jana na tayari yupo Zanzibar na kikosi huku akifanya mazoezi chini ya uangalizi wa kocha wa viungo.

Babacar amekuja Zanzibar na kuanza mazoezi moja kwa moja ili kuweza kuwazoea mapema wenzake pamoja na mazingira ili atakpoanza kupata nafasi isiwe changamoto kwake.

Kama utimamu wake utakuwa vizuri tunaweza kumuona Babacar katika michezo ya mwishoni ya michuano hii ya Mapinduzi kwa vile ambavyo kocha Abdelhak Benchikha ataona inafaa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER