Baada ya ushindi timu yaanza safari kurejea Dar

Kikosi chetu kimeanza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam usiku huu kutoka Angola baada ya ushindi mnono wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Premiero De Agosto kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu inatarajiwa kuwasili nyumbani alfajiri na wachezaji wataingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Licha ya kupata ushindi huo ugenini tunaona bado hatujamaliza mechi ndiyo maana maandalizi ya mchezo wa marudiano tunayaanza mapema.

Viingilio vya mchezo vitatangazwa mapema na vituo ambavyo tiketi zitapatikana vitawekwa hadharani ili mashabiki wanunue kwa wingi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER