Baada ya kambi ya Uturuki Robertinho autaka ubingwa

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahi ubora wa kikosi tulichonacho kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/24 huku akiweka wazi malengo yetu ni kuchukua mataji ya ndani.

Robertinho amesema kikosi chetu kina uwiano mzuri ambapo kwenye kila nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili wa kiwango cha juu.

Robertinho amesema aina ya kikosi tulichonacho tunaweza kucheza mfumo wa aina yoyote na kupata matokeo chanya.

Robertinho ameupongeza Uongozi wa klabu wa kusajili wachezaji bora huku akisema tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na kimataifa.

“Nimeridhika na kambi ya maandalizi nchini Uturuki. Tumekuwa na wiki tatu nzuri huku tukiwa na kikosi bora pia. Tuna wachezaji zaidi ya wawili kwenye kila nafasi.

“Naupongeza Uongozi wa klabu kwa kufanya usajili huu mkubwa. Simba ni timu kubwa na tuna malengo ya kuchukua ubingwa wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER