Ayoub Lakred yupo sana Simba

Mlinda mlango Ayoub Lakred amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia katika timu yetu.

Lakred raia wa Morocco tumemsajili msimu uliopita kutoka FAR Rabat na kutokana na ubora aliouonyesha tumemuongezea mkataba mpya.

Lakred ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa muhimili wa timu msimu uliopita.

Tukiwa tunaendelea kusuka kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao Lakred ni sehemu ya ujenzi wa timu ndio maana ameongezewa mkataba.

Lakred ataungana na kikosi katika kambi ya maandalizi nchini Misri moja kwa moja ambacho kitaondoka leo jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER