Augustine Okajepha ni Mnyama

Ni rasmi tumekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Augustine Okajepha raia wa Nigeria kutoka Rivers United kwa mkataba wa miaka mitatu.

Okajepha ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 20 aliyetunukiwa kipaji kikubwa katika idara ya kiungo wa ulinzi.

Katika miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihitaji kupata mchezaji ambaye ataipa uimara safu yetu ya ulinzi na Okajepha anatarajiwa kuwa suluhisho.

Okajepha ndiye mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu nchini Nigeria (MVP) msimu wa 2023/24.

2023/24 Okajepha amefunga bao moja akisaidia kupatikana mabao matatu huku mara mbili akiibuka mchezaji bora wa mwezi pamoja na kujumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Moja ya sifa kubwa ya Okajepha ni kuhakikisha eneo la ulinzi linakuwa salama muda wote wa mchezo pamoja na kupiga safi na kwenda mbele na kuongeza mashambulizi.

Ubora na umri wake ni miongoni mwa sifa zilizo tuvutia kuhitaji saini yake na tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/25.

Msimu uliopita Okajepha amechaguliwa mara mbili katika kikosi bora cha wiki cha Kombe la Shirikisho barani Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER