Ateba aanza mazoezi rasmi na wenzake

Mshambuliaji mpya Leonel Ateba amefanya mazoezi jioni pamoja na wenzake ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ajiunge na kikosi chetu.

Ateba amefanyiwa vipimo vya afya jana asubuhi na amefuzu na leo jioni amefanya mazoezi katika Uwanja wa KMC kujiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Tabora United.

Jambo jema ni kwamba Ateba amefanya maandalizi ya msimu (Pre Season) akiwa na timu yake ya USM Alger kwahiyo yupo tayari kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi.

Kwa upande wake mlinda mlango Aishi Manula nae amejiunga na kikosi na ameshiriki mazoezi ya leo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Jumapili.

Wachezaji wengine wote wameshiriki mazoezi hayo huku morali ikiwa juu tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER