Baada ya miaka mitano aliyodumu ndani ya klabu yetu mlinzi wa kati Kennedy Wilson Juma hatokuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya baada ya mkataba wake kumalizika.
Kennedy alijiunga nasi Julai 2019 akitokea Singida United na amekuwa akifanya vizuri uwanjani kila anapopata nafasi.
Kennedy ni mmoja ya wachezaji watulivu na wasikivu ndani ya kikosi chetu na amekuwa akifanya kila anachotakiwa ndani ya muda unaohitajika.
Pamoja na ubora na uwezo alionao Kennedy lakini hayupo kwenye mipango ya kusuka kikosi imara kuelekea msimu ujao wa mashindano hivyo hatukuongeza nae mkataba.
Uongozi wa klabu unamshukuru Kennedy kwa utumishi wake uliotukuka na kumtakia kheri katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.