Ally Salim Mchezaji Bora Aprili

Mlinda mlango Ally Salim, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Ally ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi zetu zilizopita amewapiku kiungo mshambuliaji Kibu Denis na mshambuliaji Jean Baleke aliokuwa anawania nao tuzo hiyo.

Katika mwezi Aprili, Ally amecheza mechi nne sawa na dakika 270 akiondoka na ‘clean sheet’ tatu akiruhusu bao moja.

Mchanguo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia

Baleke 414 22.84

Kibu 655 36.13

Ally 744 41.04

Ally anakuwa mlinda mlango wa kwanza kushinda tuzo hiyo tangu ilivyoanza kutolewa miaka miwili iliyopita.

Ally atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile ikiwa ni zawadi ya kuibuka mshindi wa kinyang’anyiro hicho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER