Mlinda mlango, Ally Salim ameibuka Shujaa wakati tukinyakua Ngao ya Jamii kwa mikwaju ya 3-1 dhidi ya watani wa jadi Yanga baada ya kuokoa tatu katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani.
Ally ameokoa penati zilizopigwa Khalid Aucho, Pacome Zouzou na Yao Attousi huku Jean Baleke akifunga penati ya ushindi.
Katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Singida Fountain Gate tulishinda kwa penati 4-2 Ally aliokoa penati moja.
Penati zetu zimefungwa na Muzamiru Yassin, Essomba Onana na Beleke huku Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri wakikosa.
Mchezo ulianza kwa kasi huku watani Yanga wakifika zaidi langoni kwetu lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Che Fondoh Malone na Kennedy Juma ilikuwa imara.
Dakika 15 za mwisho za kipindi cha kwanza tuliukamata mchezo ingawa hata hivyo mashambulizi yetu yaliishia kwa walinzi wa Yanga.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini ufanisi wa kutumia nafasi zilizopatikana ulikuwa hafifu.
Hii ni mara ya 10 kushinda Ngao ya Jamii tukiongoza kuchukua tangu ilivyoanzishwa.
X1: Diara, Yao, Lomalisa (Kibabage 76′), Baca, Mwamnyeto, Aucho, Max, Mudathir (Mkude 63′) Mzize (Konkoni 76′), Musonda (Zouzou 83′), Moloko (Aziz Ki 63′).
Walioonyeshwa kadi:
X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr (Phiri 90+3), Kennedy, Che Malone, Kanoute (Ngoma 45′), Chama (Baleke 66′) Mzamiru, Bocco (Onana 66′) Ntibazonkiza, Miquissone (Kibu 45′)
Walioonyeshwa kadi: Kennedy 51′ Mzamiru 57′