Alichosema Zoran baada ya mchezo dhidi ya Kagera

Kocha Mkuu Zoran Maki, ameweka wazi amefurahi kupata alama tatu katika mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar ingawa amekiri tumepoteza nafasi nyingi.

Zoran amesema tumepoteza nafasi nane kipindi cha kwanza na sita kupindi cha pili na mpira kumalizika kwa ushindi wa mabao mawili kitu ambacho si kizuri.

Zoran ameongeza kuwa amefurahi kuona wachezaji wapya wawili, Moses Phiri na Dejan Georgijevic wakifunga katika mchezo wa jana kitu ambacho kinawapa hali ya kujiamini.

“Nimefurahi kupata alama tatu kwenye mchezo wa jana, tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini tulipoteza nafasi nyingi ambazo zingetufanya kupata ushindi mnono zaidi.

“Tuna wiki moja na nusu ya kujiandaa kabla ya mchezo wetu unaofuata naamini tutafanya marekebisho,” amesema Kocha Zoran.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER