Alichosema Robertinho kuhusu mchezo na African Sports Kesho

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tumejipanga kuhakikisha tunashinda dhidi ya African Sports kesho ili kutinga Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Robertinho amesema siku zote malengo ya Simba ni kushinda kila taji la michuano tunayoshiriki kwa hiyo tunahitaji kupata ushindi kesho.

Amesema kesho anategemea kuwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi kubwa kikosini kwa kuwa wiki ijayo tuna mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho wa ASFC dhidi ya African Sports, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kushinda kila taji na tupo tayari.

“Tunategemea kuwatumia wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa kikosini kwa kuwa tuna mchezo wa marudiano nyumbani dhidi ya Vipers kwa hiyo tunaziangalia mechi zote,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER