Alichosema Robertinho kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Singida

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate FC yamekamilika.

Robertinho amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kimwili na kiakili kuhakikisha tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wa kesho.

Robertinho ameongeza kuwa Singida ni timu nzuri imesajili wachezaji imara lakini Simba ni kubwa na malengo yake ni kushinda taji.

“Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, wachezaji wapo vizuri. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kwa ajili ya ushindi ili tutinge fainali.

“Nafurahi kuona wachezaji wapya tuliowasajili wakiingia kikosini na kufanya vizuri. Juzi Willy Onana na Fabrice Ngoma walifunga mabao na wote ni wageni, hilo ni jambo zuri,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu.

“Ngao ya Jamii ina maana kubwa kuichukua sababu inakupa ramani kuelekea msimu mpya wa ligi utakavyokuwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kushinda,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER