Alichosema Robertinho kuelekea Mchezo wa Kesho dhidi ya Ihefu

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hao.

Robertinho amesema amepata nafasi ya kuwatazama Ihefu na kugundua wanacheza kitimu na wakati mwingine wanatumia nguvu kwahiyo tumejipanga kuhakikisha tunawakabili.

Robertinho amebainisha kuwa Simba ni timu kubwa na anawaamini wachezaji wetu hivyo tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi.

“Siku mbili nyuma nimewatazama wapinzani wetu wanacheza vizuri lakini Simba ni kubwa na tunaamini tutacheza soka safi na kupata ushindi,” amesema Robertinho.

Kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Shabani Chilunda amesema kwenye ligi kila mechi ni ngumu ila wao wamejiandaa kuhakikisha tunacheza soka safi na kushinda.

“Mechi itakuwa ngumu, tunaiheshimu Ihefu lakini tumejiandaa vizuri. Kila mchezaji atayepata nafasi atakuwa tayari kuipigania timu kupata ushindi,” amesema Chilunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER