Alichosema Robertinho kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni.

Robertinho amesema tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Coastal lakini Simba ni timu kubwa na mara zote malengo yetu ni kucheza soka safi na kushinda mechi.

Robertinho ameongeza kuwa tuna kikosi bora ambacho kinaweza kucheza na timu yoyote na anawaamini wachezaji wake wanaweza kufanya vizuri kwenye mechi ya kesho.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Coastal. Sisi kila mpinzani tunamuheshimu na tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tunahitaji kupata alama tatu.”

“Haitakuwa mechi rahisi kwakuwa Coastal wana kikosi kizuri lakini nawaamini wachezaji wangu na siku zote tunaingia uwanjani kwa kucheza soka safi na kushinda,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER