Alichosema Robertinho kuelekea mchezo dhidi ya Singida Kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Robertinho amesema amefurahishwa na hali ya kikosi ilivyo kwa sasa kwakuwa wachezaji wote waliokuwa majeruhi wamerejea uwanjani hivyo atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Robertinho ameongeza kuwa kama ilivyo kawaida tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo la kucheza soka safi la kushambulia na kukaba kwa pamoja.

“Maandalizi yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri. Jambo zuri kwangu kama mwalimu pamoja na benchi zima la ufundi ni kuona wachezaji wote wakiwa wako fiti.

“Tunategemea kupanga kikosi kamili kwakuwa tunaenda kukutana na timu bora. Tumejipanga kushinda kwakuwa tunahitaji kuwa na morali kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tutacheza kwa kufuata falsafa za Simba, tunashambulia na kukaba kwa pamoja lakini lengo letu ni kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Robertinho.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER