Alichosema Robertinho baada ya ushindi wa jana dhidi ya Vipers

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewasifia wachezaji kwa jitihada kubwa walizofanya kufanikisha ushindi wa bao moja dhidi ya Vipers katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Robertinho amesema haikuwa mechi rahisi kwakuwa Vipers walikuwa wanatupa presha mara kwa mara lakini wachezaji wetu walikuwa makini muda wote.

Robertinho ameongeza kuwa tumecheza kwa umoja kuanzia kwa walinzi, viungo hadi kwa washambuliaji na ndicho kimesababisha ushindi upatikane.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa jitihada walizofanya, tumecheza kwa umoja kuanzia nyuma hadi mbele hilo ndilo jambo zuri.

“Kwenye Ligi ya Mabingwa hakuna mechi rahisi hata sisi tulijipanga kwa hilo kutoka kwa Vipers, kinachotakiwa ni kupata pointi tatu,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER