Alichosema Robertinho baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kipanga

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema amefurahishwa na jinsi wachezaji walivyocheza katika ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kipanga FC uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Robertinho amesema kwa jinsi hali ya kikosi ilivyo inampa moyo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16.

Robertinho amesema tumecheza vizuri zaidi ya wapinzani kwa kuanzia kuzuia, kushambulia na kutumia nafasi zilizopatikana kitu ambacho kinazidi kumpa moyo.

“Timu inazidi kuimarika, tumetumia wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza na wamecheza kitimu na hilo ni jambo jema,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER