Alichosema Robertinho baada ya kutua Dar

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya licha ya kutolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 na Wydad Casablanca katika mchezo wa marudiano wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa juzi nchini Morocco.

Robertinho amesema kiwango tulichoonyesha kimekuwa gumzo kubwa kote jambo linalofanya kuwapongeza wachezaji kwa kufuata maelekezo waliyowapa.

Robertinho ameongeza kuwa kama tungezitumia vizuri nafasi tulizopata katika mchezo wa kwanza nyumbani tungefanikiwa kutinga nusu fainali lakini kwenye mpira hilo linatokea na tumerudi kujipanga.

“Tumecheza vizuri, tuliweza kuwadhibiti muda mrefu wa mchezo. Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa tuliyofanya.”

“Kiwango tulichoonyesha kinazungumziwa kila mahali, hilo ni jambo zuri, tumerudi nyumbani kujipanga na michuano iliyo mbele yetu,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER