Alichosema Pablo kuhusu mchezo dhidi ya Azam

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakuwa na burudani kutokana na aina ya wachezaji wa timu zote pamoja na uwanja utakaotumika.

Pablo amesema tuna wachezaji wazuri katika kila idara kama ilivyo kwa Azam hivyo anatarajia mchezo mzuri kutokana na Uwanja wa Azam Complex ambao utatumika kuwa bora katika eneo la kuchezea.

Pablo ameongeza kuwa katika mechi zetu zilizopita tuliwakosa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kutokana na kuwa majeruhi lakini baadhi wamerejea na wapo tayari kwa mechi ya kesho.

“Kwetu sisi kila mchezo ni fainali tunahitaji kushinda ili kuendelea kupunguza tofauti ya alama zilizopo na vinara. Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam lakini tupo tayari kupambania pointi tatu.

“Tuliwafunga mchezo wa mzunguko wa kwanza na kwenye Kombe la Mapinduzi pia lakini haimaanishi itakuwa rahisi bali tutapambana,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER