Alichosema Pablo kuelekea mchezo wa kesho

Kocha Mkuu Pablo Franco, amefunguka kuwa lengo ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo uliopo mbele yetu katika Michuano ya Mapinduzi ili kuibuka mabingwa.

Pablo amesema anaamini yeye siku zote ni mshindi hivyo kila mchezo anapenda kupata ushindi bila kujali anacheza nani.

Raia huyo wa Hispania amesema mchezo wa kesho dhidi ya Selem View utakuwa mgumu lakini kwa maandalizi yetu anaamini tutaibuka na ushindi.

“Tunahitaji kushinda kesho ili kufuzu nusu fainali hilo ndilo lengo kuu. Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa mechi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER