Alichosema Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Sokoine yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema tunaiheshimu City na tunategemea kupata ushindani mkubwa hasa katika uwanja wa Sokoine lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

Mgunda amesisitiza kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu imejipanga kushinda kwahiyo kila mchezo tumeupa muhimu mkubwa.

“Tunaiheshimu Mbeya City, ni timu nzuri na imejipanga vizuri lakini nasi tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani na tupo tayari kwa mpambano.

“Kila siku nasema ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu imejipanga kupata matokeo mazuri hasa wakiwa nyumbani lakini nasi tupo tayari kwa vita ya dakika 90 kesho,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER