Alichosema Mgunda kuelekea mchezo dhidi ya Coastal kesho

Kocha msaidizi, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 9:30 Alasiri yamekamilika na kila kitu kinaenda sawa.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wa mwisho wa kufungia msimu wa Ligi 2022/23.

Mgunda ameongeza kuwa itakuwa mechi ngumu kwakuwa Coastal watahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo nasi malengo yetu ni kumaliza ligi vizuri.

“Maandalizi kwa ajili ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa kuipambania timu kupata alama tatu.

“Tunajua itakuwa mechi ngumu, Coastal ni timu nzuri na inahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri nasi malengo yetu ni kushinda kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER