Alichosema Mgunda baada ya sare dhidi ya Namungo

Kocha Msaidizi Juma Mgunda, amesema baada kupata sare ya kufungana bao moja dhidi ya Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Majaliwa lengo letu sasa ni kuhakikisha tushinda mechi zilizosalia.

Mgunda amesema bila kujali matokeo ya timu nyingine sisi tutahakikisha tunafanya kila linalowezekana kupata alama tatu katika kila mchezo uliobaki ili kumaliza vizuri msimu wa ligi.

Mgunda ameongeza kuwa kabla ya kuingia kwenye mchezo dhidi ya Namungo tulifahamu utakuwa mgumu na tulikuwa tumejiandaa lakini kilichotokea ni sehemu ya mpira na tunajipanga kwa mchezo ujao.

“Mchezo dhidi ya Namungo umemalizika tumepata sare, tunarudi uwanja wa mazoezi kujiandaa na mechi zilizosalia. Sisi hatuangalii nani kafanya nini tunahitaji kushinda mechi zetu zote.

“Tulijua isingekuwa mechi rahisi, Namungo ni timu nzuri hasa inapokuwa nyumbani lakini mpira una matokeo matatu tunarudi kujipanga kwa mechi zilizo mbele yetu,” amesema Mgunda.
[08:41, 04/05/2023] Kichico: Ally Salim Mchezaji bora Aprili

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER