Alichosema Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kagera

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Matola amesema mchezo utakuwa mgumu na tutaingia kwa kuwaheshimu Kagera kutokana na ubora wao lakini tupo tayari kuwakabili.

Matola ameongeza kuwa mara zote tunapokutana na Kagera mchezo unakuwa mgumu lakini safari hii tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu katika uwanja wa nyumbani.

“Kikosi kipo tayari tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa kutokana na majeraha au sababu yoyote, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari,” amesema Matola.

Kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kuwapa sapoti wachezaji na anaamini tutawalipa kwa furaha.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo, tumepata maandalizi mazuri kutoka kwa walimu wetu kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani tunaamini tutawapa furaha,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER