Alichosema Matola baada ya ushindi dhidi ya Jamhuri

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema tulistahili kupata ushindi mnono zaidi kama tungezitumia vizuri nafasi tulizotengeneza.

Matola amesema tumetengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza lakini hatukuweza kuzitumia vizuri.

Matola ameongeza Jamhuri walicheza kwa nidhamu hasa kwenye kuzuia ambapo walikuwa wengi kwenye eneo lao huku wakiziba mianya katika kila eneo.

“Ilikuwa mechi ngumu, katika hatua kama hii ambayo ukipoteza unatoka timu zinatumia mbinu nyingi.”

“Wenzetu Jamhuri walikuja na mbinu ya kukaa nyuma kutusubiri huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza. Tulistahili zaidi ya ushindi tuliopata sababu tumetengeneza nafasi nyingi,” amesema Matola.

Kuhusu mchezo wa nusu fainali ambao tutacheza dhidi ya Singida Fountain Gate siku ya Jumatano, Matola amesema “kesho tutafanya mazoezi na maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER