Alichosema Matola baada ya kumaliza kozi

Kocha wetu msaidizi Seleman Matola ni miongoni mwa washiriki 25 waliohitimu kozi ya Diploma B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyofungwa leo mkoani Morogoro.

Matola amesema anashukuru kwa kumaliza salama kozi na anarejea kikosini kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kuelekea michuano iliyo mbele yetu.

Matola ameendelea kuwaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi uwanjani katika kila mchezo ili kuwapa sapoti wachezaji huku akiwashukuru kwa jinsi walivyokuja katika mechi iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania.

“Namshukuru Mungu tumemaliza kozi salama na nimerejea kuungana na benchi la ufundi tayari kwa mapambano yaliyo mbele yetu, kikubwa ninachoomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kwenye mechi zetu kutupa sapoti,” amesema Matola.

Matola ataungana na kikosi katika mazoezi ya mwisho ya kesho ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union yatakayofanyika Uwanja wa Boko Veterans na Jumapili atakuwepo kwenye benchi la ufundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER