Alichosema Kocha Robertinho kuelekea mchezo wetu dhidi ya Wydad

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kikosi chetu kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Robertinho amesema tutaingia katika mchezo huo kwa lengo moja la kuhakikisha tunacheza vizuri pamoja na kupata ushindi wa nyumbani.

Robertinho amesema amewasisitiza wachezaji kuhakikisha wanacheza vizuri zaidi tukiwa hatuna mpira kwa kuwa itakuwa rahisi kuwasoma wapinzani.

Robertinho amekiri mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu Wydad kutokana na ubora wao na historia yao lakini tumejipanga kikamilifu na tuko tayari kwa mchezo.

“Katika Ligi ya Mabingwa hakuna timu nyepesi, Wydad ni timu bora kama ilivyo Simba na nyinginezo. Tumefanya maandalizi mazuri na timu ipo tayari kwa mchezo.

“Tumewasisitiza wachezaji kucheza vizuri tukiwa na hatuna mpira kwa sababu itatusaidia kuwasoma wapinzani, tunahitaji kushinda sanjari na kucheza vizuri,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER