Alichosema Kocha Pablo kabla ya kuifuata Ruvu Shooting

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa tunahitaji kupata alama tatu katika mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Ijumaa ili kuongeza hali ya kujiamini kikosini.

Kauli hiyo ameitoa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kupaa kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Pablo amesema ingawa hajapata muda mrefu wa kufanya mazoezi pamoja na wachezaji lakini anaamini tutapambana kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu.

Pablo ameongeza kuwa kurejea kwa nyota waliokuwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kumeongeza nguvu kikosini na kuelekea mchezo huo.

“Tunahitaji kupata alama tatu katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, tunajua utakuwa mgumu na upinzani utakuwa mkubwa lakini ushindi ndiyo kitu tunachohitaji ili kurudisha hali ya kujiamini,” amesema Pablo.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza wa Kocha Pablo tangu alipotua kuchukua mikoba ya Didier Gomes wiki iliyopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER