Alichosema Kocha Pablo baada ya mechi dhidi ya Mlandege

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema Mlandege walicheza kitimu hasa katika kuzuia ingawa pia walitumia zaidi nguvu kwa wachezaji wetu.

Pablo amesema michuano ya Mapinduzi ni mizuri lakini wachezaji hawalindwi ipasavyo na waamuzi kutokana na kufanyiwa rafu nyingi wakati tuna michuano mikubwa zaidi ya hii.

Pablo amesema katika mechi mbili tulizocheza kumekuwa na rafu ambazo zinawaumiza wachezaji huku waamuzi wakichukulia kawaida na inaweza kuleta madhara ambayo yataigharimu timu.

“Katika mechi mbili nimeona wachezaji wanafanyiwa rafu lakini waamuzi hawachumaamuzi yanastahili. Katika mashindano haya sio ya kuumiza wachezaji,” amesema Pablo

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER