Alichosema Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho

 

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni dhidi ya Nyasa Big Bullets yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hakuna ambaye atakosekana kutokana na sababu yoyote.

Mgunda ameongeza kuwa kiungo mkabaji Sadio Kanoute ambaye alikosekana katika mchezo uliopita nchini Malawi na ule wa Prisons kutokana kuumwa jino lakini sasa yupo tayari kwa mchezo wa kesho.

“Maandalizi ya mchezo wa kesho yamekamilika kikubwa tuwaombee wachezaji waamke salama watimize majukumu yao, Kanoute ambaye alikosekana mechi mbili zilizopita nae yupo tayari kwa mechi ya kesho,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kwa upande wao wachezaji wapo tayari kufuata malekezo waliyopewa na benchi la ufundi ili kuhakikisha tunafanya vizuri na kufuzu hatua inayofuata.

“Kama alivyosema mwalimu, maandalizi yamekamilika nasi kama wachezaji tutahakikisha tunapambana kufanya vizuri kufuzu hatua hii,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER