Alichosema Kocha Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mashujaa

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema tunaamini mchezo wa kesho dhidi ya Mashujaa FC utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

Matola amesema wachezaji wote tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunapambana hadi mwisho pamoja na ugumu utakaojitokeza ili kupata ushindi.

Matola ameongeza kuwa Mashujaa watahitaji kufanya kila linalowezekana kupata ushindi ili kujinasua katika nafasi waliyopo kwenye msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Tunajua haitakuwa mechi rahisi, Mashujaa imefanya usajili mzuri na wachezaji wengi ni wazoefu wa ligi lakini tumejipanga kuwakabili na lengo ni kupata pointi tatu.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Israel Patrick amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Lake Tanganyika kesho kuwapa sapoti ili malengo ya kupata ushindi yafikiwe.

“Sisi wachezaji tupo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho, tunafahamu itakuwa mechi ngumu. Pamoja na Mashujaa kutokuwa katika nafasi nzuri lakini tumejipanga kuwakabili kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutupa sapoti,” amesema Israel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER