Alichosema Kocha Gomez baada ya ushindi dhidi ya Kagera

Kocha Mkuu, Didier Gomez amefurahishwa na ushindi wa mabao 2-0 tulioupata dhidi ya Kagera Sugar huku akiwamwagia sifa wachezaji kwa kuonyesha kiwango kizuri.

Gomez amesema tulihitaji kupata ushindi huu ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo itakuwa ni mara ya nne mfululizo kama tutafanikiwa.

Akizungumzia mchezo wenyewe Gomez amesema tulimiliki sehemu kubwa hasa kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi huku kipindi cha pili tukipunguza kasi na kuifanya mechi kuwa na uwiano sawa.

“Nimeridhishwa na uchezaji pamoja na viwango vya wachezaji wangu, tuliweza kumiliki mpira kwa muda mrefu na jambo la kufurahisha zaidi ni kupata pointi zote tatu ugenini,” amesema Kocha Gomez.

Wakati huo huo Kocha Gomez amesema litakuwa ni jambo jema kama tutafanikiwa kushinda katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Gwambina ili kurejea jijini Dar es Salaam tukiwa na alama zote tisa kutoka Kanda ya Ziwa kama tulivyoazimia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER