Alichosema Kocha Fadlu kuelekea mchezo dhidi ya Azam

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku yamekamilika.

Fadlu amesema tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo wa kesho ingawa tunafahamu utakuwa mgumu kutokana na uimara wa Azam huku pia ikiwa ni ‘Dabi’.

Fadlu ameongeza kuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza tulipata ushindi wa mabao mawili lakini tunaamini Azam watakuja kwa nia ya kutaka kulipa kisasi ndio maana tumewaandaa wachezaji kimbinu na kiakili.

“Maandalizi ya mchezo mkubwa wa Dabi yamekamilika, tumejiandaa vizuri kimbinu za kuikabili timu bora yenye kocha bora ya Azam FC,” amesema Kocha Fadlu.

Nae nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha ushindi unapatikana na kuendelea kusogelea malengo tuliyojiwekea.

“Kwa niaba ya wachezaji naweza kusema tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, leo tutafanya mazoezi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kujiweka sawa kabla ya kushuka dimbani,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER