Alichosema Kocha Benchikha baada ya kutua nchini

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema amefurahi kuiongoza Simba na amejipanga kuivusha kuitoa hapa ilipo na kuipandisha juu.

Benchikha ametua nchini usiku huu kutoka nchini Algeria tayari kuanza kibarua cha kukionoa kikosi chetu.

Benchikha amesema lengo lake kubwa ni kuifanya timu ipate ushindi uwanjani pamoja na kupata mataji.

Benchikha ameongeza kuwa ili timu iweze kupata mafanikio lazima kuwepo na mshikamano baina ya timu, viongozi na mashabiki kwa ujumla.

“Nina furaha kuwa hapa leo, Simba ni timu kubwa Afrika, nina furaha kuwa sehemu ya historia ya kuwepo hapa.

“Tupo hapa kwa ajili ya mashabiki wa Simba, tunatakiwa kuwa imara ili kuvuka katika hali hii, tupo tayari kuwapa kiwango bora uwanjani,” amesema Benchikha.

Benchikha ameambatana na Farid Zemiti ambaye anakuwa kocha msaidizi na Kamal Boudjenane ambaye ni kocha wa viungo na wote wanatoka nchini Algeria.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER