Alichosema Benchikha baada ya ushindi dhidi ya Kagera

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amewasifu wachezaji kwa kucheza vizuri katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Benchikha amesema uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono.

Aidha Benchikha amesema Kagera ni timu nzuri na walitupa ushindani mkubwa lakini tulikuwa bora na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu. Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi

“Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” amesema Benchikha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER