Alichosema Benchikha baada ya kutua Dar

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema tulipopoteza mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Al Ahly tuliongeza ugumu mechi ya marudiano na ndio maana tumetolewa.

Benchikha amesema Al Ahly ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu ambao wanaweza kubadili mchezo muda wowote na hilo limetugharimu.

Benchikha ameongeza kuwa mchezo wa kwanza tulipoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingetuongezea hali ya kujiamini lakini hatukuzitumia na wenzetu walipata moja pekee na wameitumia hiyo hiyo.

Aidha Benchikha ameongeza kuwa anaamini msimu ujao tukishiriki michuano hii tutakuwa bora zaidi kwakuwa tutakuwa tumejifunza mengi.

“Nafikiri tulipopoteza mechi ya kwanza nyumbani ndipo tulipoongeza ugumu wa mechi ya marudiano, Al Ahly ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu wa michuano hii.”

“Tumejifunza na naamini tutakuwa bora katika michuano hii mwakani kama tukipata nafasi ya kushiriki,” amesema Benchikha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER