Alichosema Ally Salim baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya Aprili

Mlinda mlango, Ally Salim amewashukuru wachezaji wenzake pmaoja na mashabiki kwa kumuwezesha kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Ally amesema ni jambo la furaha kwakwe kushinda tuzo hiyo akiweka historia ya kuwa mlinda mlango wa kwanza kuitwaa.

“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu, nawashukuru wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki kwa kunipigia kura mpaka kushinda,” amesema Ally.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Emirate Aluminium, Issa Maeda amempongeza Ally kwa kuonyesha kiwango bora mwezi Aprili na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.

“Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ihefu ukaja dhidi ya Yanga na hata ule wa nyumbani na Wydad Casablanca alionyesha kiwango bora na tunampongeza kwa hilo.”

“Mara kadhaa Aishi Manula amewahi kuingia fainali ya kinyang’anyiro hiki lakini alizidiwa na wachezaji wa ndani ila Ally Salim ameweza na kuweka historia,” amesema Maeda.

Ally amekabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER