Alichosema Ahmed kabla ya timu kuelekea Dodoma

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.

Ahmed amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na kimepata siku mbili za kufanya mazoezi baada ya mchezo dhidi ya Kagera na wapo tayari kwa ajili ya mechi ya kesho.

Ahmed ameongeza kuwa nyota wetu watatu Clatous Chama na Luis Miquissone wamefanya mazoezi pamoja na wenzao na afya zao zimetengemaa.

Hata hivyo Ahmed amesema nyota hao hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kwakuwa tunahitaji warudi wakiwa kamili hivyo wataonekana katika mechi tatu zilizosalia.

“Tunaelekea Dodoma tukiwa tupo Kamili, kikosi kipo tayari. Tunamshukuru Mungu tulipata siku mbili za mazoezi na leo jioni tutafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani hapo kesho.”

“Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri lakini wale waliotoka kwenye majeraha hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER