Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema usajili wa kiungo mkabaji, Babacar Sarr utaenda kutibu matatizo yote ya kiulinzi ya timu yetu.
Ahmed amesema katika miaka ya karibuni tumekuwa tukikosa namba sita asilia lakini baada ya Sarr kutua tatizo limetatuliwa.
Ahmed ameongeza kuwa tangu alivyoondika James Kotei, Gerson Fraga na Taddeo Lwanga hatujawahi kupata kiungo halisi wa ukabaji ndio maana tumepambana kupata saini ya Sarr.
“Sarr ni mchezaji ambaye tulikuwa tunamkosa katika timu yetu kwa muda mrefu. Tumekuwa na wachezaji wengi bora lakini hakutuwa na namba sita halisi.”
“Sasa pale kati patakuwa na Sarr, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis, imani yetu ni kwamba tutakuwa na safu bora sana ya kiungo,” amesema Ahmed.