Alichokisema Kocha Matola kuelekea mechi na Polisi Tanzania

Kocha msaidizi Seleman Matola amesema wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa kwenye  Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, dhidi ya Polisi Tanzania.

Matola amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na tangu Jumatano tulipowasili jijini Mwanza baada ya kufanya mazoezi na kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo.

Matola ameongeza kuwa dhamira yetu ni kuhakikisha tunashinda katika michezo yetu mitatu ijayo ya ligi ili kutangazwa mabingwa tukianza na mchezo wa kesho dhidi ya maafande hao wa polisi.

“Kikosi kipo kamili wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunawaheshimu Polisi mara zote tukikutana wanatupa ushindani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Tumewafunga katika mechi zote tatu za ligi tulizokutana nao, mbili za msimu uliopita na moja msimu huu lakini haimaanishi mechi ya kesho itakuwa rahisi kwetu, tutaingia kwa tahadhari na lengo letu ni kushinda ili kusogelea ubingwa wa ligi,” amesema Matola.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema morali za wachezaji zipo juu na jambo pekee lililo vichwani mwao ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu na lengo la kila mmoja ni kuhakikisha tunashinda ili kutetea ubingwa hivyo yeyote atakayepewa nafasi atafanya hivyo,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. I believe on my time they will do better tomorrow.. All the best my team 🏏⚽⚽⚽⚽⚽ #Simba nguvu moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER