Alichokisema Bocco baada ya kutua Botswana

Nahodha wa timu yetu, John Bocco amesema wachezaji wote waliosafari kuelekea nchini Botswana wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumapili.

Bocco ameyasema hayo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaborone akiwa tayari na wachezaji wenzake kwa ajili ya mchezo huo wa mkondo wa kwanza.

Bocco ameweka wazi kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na aina ya wapinzani tunaoenda kukutana nao lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

Nahodha Bocco ameendelea kusema kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunavuka hatua ya robo fainali ambayo tuliishia msimu uliopita ili kuendelea kuitangaza Simba kimataifa.

“Maandalizi yamekamilika, wachezaji wote tuliosafiri tupo kwenye hali nzuri, vichwani mwetu tunajua mchezo utakuwa mgumu na tumejiandaa kupambana lengo ni kuvuka hatua hii,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER