Alama tatu tu dhidi ya Prisons leo

Kikosi chetu kitashuka leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utaanza saa moja usiku.

Katika mchezo wa leo tunahitaji alama tatu kwa hali yoyote ile.

Hatukuwa na matokeo mazuri katika mechi zetu tatu zilizopita hivyo pointi tatu katika mchezo wa leo zitakuwa na maana kubwa kwa timu.

Ingawa mpira una matokeo matatu na tunafahamu haitakuwa mechi nyepesi lakini tutapambana kwa hali zote.

HALI YA KIKOSI

Kocha Msaidizi Selemani Matola, amesema maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri morali ipo juu na kila mmoja yuko tayari kwa mechi.

Matola amesema anajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na Prisons kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo hivyo watahitaji kupambana ili kupata pointi tatu hatua ambayo tumejipanga kuhakikisha tunaizuia.

“Haiwezi kuwa mechi nyepesi, Prisons iko kwenye hali ngumu. Watatumia nguvu kubwa kutafuta alama tatu ili wajinasue lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda, hata sisi pointi tatu tunahitaji kupunguza tofauti na aliyejuu yetu,” amesema Matola.

GADIEL AWAITA MASHABIKI

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael, amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kutoa sapoti na wachezaji ambapo watawalipa kwa furaha ya ushindi.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wa leo, kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi tunaamini tutawapa furaha kwa ushindi,” amesema Gadiel.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER