Al Hilal Kutua Dar Kesho kwa mwaliko wa Simba

Mabingwa wa soka nchini Sudan, Al Hilal watatua jijini Dar es Salaam kesho saa sita mchana kwa mwaliko maalumu kutoka kwetu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Wakiwa jijini Dar es Salaam, Al Hilal watacheza mechi tatu za za kirafiki dhidi ya Namungo, Azam FC na sisi wenyeji Simba.

Maandalizi yao yote kuanzia kesho watakapowasili nchini yatakuwa juu yetu ikiwemo mahali watakapofikia, uwanja wa mazoezi na vingine vyote mpaka siku watakayoondoka nchini Februari 6, mwaka huu.

Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu amesema tuliingia mkataba wa ushirikiano wa Al Hilal na moja ya makubaliamo ni kutembeleana na kufanya mashindano ili kuimarisha vikosi vyetu.

“Mtakumbuka mwaka 2021 tuliwaalika Al Hilal kwenye Muichuano ya Simba Super Cup na mwaka jana wao waliandaa nasi tukashiriki, kwa hiyo ushirikano wetu unaendelea vizuri,” amesema Mangungu.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Al Hilal, Elfadhili Hussein ameushukuru uongozi wa klabu kwa kuendeleza ushirikiano na wanaamini watapata mazoezi mazuri kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mamelodi.

“Baada ya kupata ratiba hii tuliwasiliana na Simba ili tuje tuweke kambi Tanzania, tuwashukuru Simba ikakukabli na kuandaa kila kitu. Tunaamini tutapata maandalizi mazuri,” amesema Elfadhili.

Ratiba ya mechi za Al Hilal

Januari 26, Namungo vs Al Hilal (Azam Complex)

Januari 31, Azam vs Al Hilal (Azam Complex)

February 5, Simba vs Al Hilal (Benjamin Mkapa)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER