AJIBU ATUPIA MAWILI TUKIITUPA NJE LYON FA

Kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu amefunga mara mbili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na kuwatupa nje ya mashindano.

Ajibu alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya na kuwapita walinzia wa Lyon na mlinda mlango wao kabla ya kumkuta mfungaji.

Fundi huyu wa mpira alitupatia bao la pili dakika ya 42 kufuatia shuti la Bwalya kuokolewa na mlinda mlango wa Lyon kabla ya mpira kumkuta akiwa ndani ya 18.

Perfect Chikwendwe alikamilisha karamu ya mabao baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 62 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Miraji Athumani aliyetokea benchi.

Ushindi huu unatufanya kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hii ambayo sisi ndio Mabingwa watetezi kufuatia kulinyakua taji hilo msimu uliopita.

Kikosi kitashuka dimbani siku ya Jumatatu kuikabili JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER