Aisha Mnuka atupia hat trick Queens ikichapa Amani Ilulu

Mabao matatu yaliyofungwa na mshambuliaji Aisha Mnuka yametupa ushindi wa 3-2 dhidi ya Amani Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa Ilulu.

Licha ya kufunga mabao hayo Aisha alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Amani na kuwafanya wawe nae makini muda wote.

Aisha alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 48 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Bao hilo halikudumu kwani Amani walisawazisha dakika ya 50 kabla ya kuongeza la pili muda mfupi baadae lakini Mnuka aliongeza la pili dakika ya 55 kufuatia Asha Djafar kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Dakika ya 90 Aisha alikamilisha ‘hat trick’ kwa kufunga bao la tatu baada ya kupiga shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Amani Queens Asha Mrisho.

Hii ni hat trick ya pili ya Aisha baada ya ile ya kwanza tuliobuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ceasiaa Queens.

Kocha Musa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Danai Bhobho, Ritticia Nabbosa na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Esther Mayalla, Jentrix Shikangwa na Mwanahamisi Omary.

Mchezo huo unatufanya kufikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zetu zote za ligi tulizocheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER