Ahsante Peter Banda

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na Winga Peter Banda.

Banda (23) alisajiliwa Agosti 3, mwaka 2021 kutoka Nyasa Big Bullets ya nchini kwao Malawi kwa mkataba wa miaka mitatu.

Katika kipindi cha miaka miwili tulichokuwa na Banda amekuwa mchezaji muhimu ambaye alikuwa akiongeza kasi katika safu ya ushambuliaji.

Uongozi wa klabu unathamini mchango wa Banda kwenye timu katika kipindi chote alichodumu nasi.

Simba inamshukuru na kumtakia heri Banda katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER