Ahmed: Wanasimba msiingie unyonge, Twendeni Kwa Mkapa Jumamosi

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amewaomba Wanasimba kutokata tamaa na kuingia unyonge baada ya kupata matokeo mabaya kwenye mechi zetu mbili za ligi zilizopita.

Ahmed ameyasema hayo katika Tawi la Full Squard Mwananyamala Mchangani ‘Moto wa Tipa’ wakati wa zoezi la hamasa kuelekea mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25.

Ahmed amesema malengo ya timu ni kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ni kufika nusu fainali na hilo litawezekana endapo tutakuwa na mshikamano.

Ahmed amewaomba Wanasimba kutoka Mwananyamala kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi kwakuwa tunahitaji kupata pointi tatu nyumbani kutoka ASEC.

“Wanasimba tusiishi kinyonge, tumewahi kupitia magumu kuliko hivi tukasonga mbele mpaka sasa tupo nafasi ya nane Afrika.

“Novemba 25 ni siku ya kurejesha heshima, wengi wana subiri tupoteze ili wapate cha kusema lakini twendeni uwanjani tukawape pumzi ya moto ASEC na kuanza vizuri hatua ya makundi,” amesema Ahmed.

Malengo yatatimizwa endapo Wanasimba tutakuwa pamoja. Wanasimba tushikamane tuhakikishe tunachukua pointi tatu.

Akizungumzia mchezo dhidi ya ASEC Ahemd amesema “tuliwahi kuwafunga mabao matatu hapa hapa kwa Mkapa kwahiyo hatujifunzi jinsi ya kumfunga kwakuwa tunajua jinsi ya kufanya na tutafanya hivyo Jumamosi.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER