Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi Novemba 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.
Ahmed amesema tunajua mashabiki wameumia baada ya matokeo mabaya tuliyopa katika mechi zetu mbili zilizopita lakini hatupaswi kuitelekeza timu yetu.
Kutokana na mchango mkubwa wa mashabiki ambao wametufanya kupata tuzo katika michuano ya African Football League (AFL) katika mechi dhidi ya ASEC hivo uongozi wa Simba umewapa heshima kubwa ya kuwa Mgeni rasmi katika mchezo huo.
Ahmed ameongeza kuwa ushindi katika mchezo dhidi ya ASEC hautapunguza machungu yetu bali utatuweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.
“Tunajua mashabiki wetu wameumia, sisi viongozi tumeumia na wachezaji pia kwahiyo tunapaswa kusahau yaliyopita na kusonga mbele.
“Tunahitaji wingi wa mashabiki Novemba 25 kwa Mkapa, ASEC ni timu bora kwahiyo mashabiki ni watu muhimu ambao wana mchango wa kuhakikisha tunarejesha ari ndani ya timu.”
Ahmed ameongeza kuwa “ukijiona umefika Uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 25 ujue wewe ni mgeni rasmi wa mchezo wetu dhidi ya ASEC.”
One Response
Tunataka mabadiliko ya Team kama bado kuna migogoro yaishe mapema kuna mambo muhim yatakiwa kufanyika kwa wakati tuweze kufika clab bingwa fainal